Kikao kilihitimishwa kwa dua na nasaha za mwisho kutoka kwa Sheikh, akiwatakia Wanafunzi mafanikio katika safari yao ya elimu na kutafuta maarifa yanayofaa kwa maisha ya duniani na Akhera.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo Jumamosi, 26 Julai, 2025 - Kikao maalumu cha kielimu kuhusu Umuhimu wa Kujifunza Historia na Nafasi yake katika "Wakati wa Sasa" kimefanyika katika kituo cha Kielimu cha Jamiat Al-Mustafa (s), Dar es Salaam, kwa ushiriki wa Wanafunzi wa Elimu ya juu na Wapenzi wa Historia na masuala ya kijamii.
Hujjatul Islam wal Muslimin Sheikh Abdul Majid Nasir, ndiye aliyewasilisha Mada hiyo katika kikao hicho.
Katika mazungumzo yake, alieleza kuwa:
"Kujifunza historia ni kulinda kumbukumbu ya ustaarabu wa jamii. Historia ni taa ya kutuongoza leo kwa misingi ya yaliyotokea jana. Taifa lisilojifunza kutoka kwa historia lina hatari ya kurudia makosa yale yale."
Aidha, alibainisha kuwa historia ya Kiislamu ni hazina kubwa ya mafunzo na mazingatio, yanayoweza kusaidia katika kuijenga jamii ya maarifa, maadili na mwamko wa kiroho.
Baada ya hotuba, kikao kiliendelea kwa kipindi cha maswali na majibu ambapo wanafunzi waliuliza maswali mbalimbali na kushiriki katika mijadala ya kina na mzungumzaji, jambo lililochangia kuongeza hamasa na uelewa wa pamoja.
Kikao kilihitimishwa kwa dua na nasaha za mwisho kutoka kwa Sheikh, akiwatakia Wanafunzi mafanikio katika safari yao ya elimu na kutafuta maarifa yanayofaa kwa maisha ya duniani na Akhera.
Your Comment